#Business

MAUZO YA KENYA KWA MATAIFA MENGINE YAONGEZEKA; CBK YASEMA

Benki kuu ya Kenya CBK katika ripoti ya kiuchumi imesema mauzo ya taifa hili kwa nchi nyingine za Afrika yameongezeka kwa asilimia 16.5 ambayo ni sawa na shilingi bilioni 113.1 katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 kutoka dola milioni 749 ya mwaka 2023 kipindi sawa na hicho.

Kulingana na CBK mafanikio hayo yametokana na sera ya serikali kuu kuruhusu watu kutoka nchi zote za Afrika kuingia nchini kupitia mipaka yake bila vizingiti vyovyote tangazo ambalo lilitolewa na utawala wa  rais William Ruto mwezi Desemba mwaka 2023.

Ripoti hiyo imesema bidhaa nyingi kutoka taifa hili ziliuzwa nchini Uganda, Tanzania na Rwanda, huku Misri, Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zikiwa na mahitaji makubwa.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *