#Football #Sports

ARSENAL YAKARIBIA KUFUZU LIGI YA MABINGWA BAADA YA SARE YA 2-2 NA LIVERPOOL

Arsenal walikubaliana na Liverpool kwa sare ya 2-2 baada ya kurudi kutoka nyuma kwa mabao mawili, wakijikatia tiketi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa.

Liverpool waliongoza kwa mabao ya Cody Gakpo na Luis Diaz, lakini Gabriel Martinelli alifunga bao la kwanza la Arsenal, na Mikel Merino kusawazisha. Ingawa Merino alionyeshwa kadi nyekundu, Arsenal walishikilia sare muhimu katika kinyang’anyiro cha kumaliza nafasi tano za juu.

Arsenal wako nafasi ya pili, wakiwa na pointi tano mbele ya Aston Villa, na wanajiandaa kukutana na Newcastle kwenye Uwanja wa Emirate’s wiki ijayo kabla ya kutembelea Southampton kwenye siku ya mwisho ya msimu.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *