KENYA KUPELEKA MAAFISA 600 ZAIDI WA POLISI NCHINI HAITI – RUTO
Maafisa wengine 600 wa polisi wa Kenya wanatarajiwa kujiunga na wenzao nchini Haiti ili kupiga jeki juhudi za kukabilia na wahalifu.
Maafisa hao kwa sasa wanaendelea na mafunzo na watakuwa tayari kwa kazi nchini Haiti hivi karibuni,
Kenya inaongoza mwitikio wa kimataifa kwa wito wa dharura wa Haiti wa kuungwa mkono katika kurejesha usalama nchini humo.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliidhinisha kutumwa kwa Ujumbe wa Kimataifa wa Msaada wa Usalama (MSS) nchini Haiti mnamo Oktoba 2, 2023.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































