MSHUKIWA MKUU WA WIZI WA MTIHANI WA KCSE AKAMATWA HUKO NAKURU

Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imemkamata mwanamume anayedaiwa kuwa mmoja wa wahalifu wanaotafutwa sana nchini Kenya kwa kuhusika na udanganyifu wa mtihani wa KCSE wa 2024 na anatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo.
Kulingana na dci Collins Kipchumba Kemboi mwenye umri wa miaka 23 anashirikiana na Dorothy Jerop Kiprono kuendesha mifumo ya uvujaji wa mitihani kwenye mitandao yaTelegram na WhatsApp,
Inadaiwa ana wafuasi zaidi ya 78,000 kwenye Telegram na zaidi ya 8,500 katika vikundi vyake vya WhatsApp.
Imetayarishwa na Janice Marete