#Football #Sports

HUSSEIN ATAKA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI

Huku uchaguzi unaosubiriwa kwa hamu na Shirikisho la Soka la Kenya FKF ukikaribia, Hussein Mohamed, mmoja wa wanaowania kiti cha urais, ametoa wito wa uchaguzi huru na wa haki.

Akizungumza mjini Iten, Elgeyo Marakwet wakati wa fainali za kombe la Gavana wa Raia, Mohamed alisema kuzinduliwa kwa bodi ya uchaguzi kunafaa kuhakikisha kunaandaliwa uchaguzi wa kuaminika, ili kuhakikisha soka inasimamiwa vyema nchini.

FKF mnamo Jumatatu ilizindua bodi ya uchaguzi ambayo itaongozwa na Heson Owilla. Owilla, katika hotuba yake, alisema wanalenga kukamilisha zoezi hilo katikati ya mwezi Desemba.

Iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa FKF, Mohamed alisema atahakikisha timu ya taifa ya kandanda Harambe Stars inapata mafanikio makubwa zaidi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HUSSEIN ATAKA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI

BRAD IBS AFURAHISHWA NA KIKOSI CHAKE

HUSSEIN ATAKA UCHAGUZI WA HURU NA HAKI

HATUA ZA KIDHARURA ZICHUKULIWE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *