TIMIZENI AHADI, WALIMU KWA SERIKALI
Huku ikisalia takribani miezi 2 kabla ya masomo ya gredi ya 9 kuanza, muungano wa walimu wa shule za msingi umeitaka serikali kuwaajiri walimu zaidi watakaofanikisha masomo hayo jinsi iliyoahidi.
Wakizungumza jijini Mombasa wakati wa kongamano lao la kila mwaka, wlaimu hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Johnson Nzioka wamesema utekelezwaji wa masomo ya sekondari msingi unakumbwa na uhaba wa walimu.
Aidha, wameihimiza serikali kukamilisha ujenzi wa madarasa 18,0000 ya gredi ya 9.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































