UMEME MASHINANI KAUNTI YA KISII

Wananchi wamehimizwa kulinda nyaya za umeme na kuripoti visa vya wizi wa nyayo hizo ili kupunguza visa vya kujpotea kwa umeme kila mara
Akizungumza baada ya kuzindua mradi wa ujenzi wa mfumo wa umeme kaunti ya kisii seneta maalum Esther Okenyuri ameelezea umuhimu wa wananchi kuwa mstari wa mbele kulinda vifaa hivyo kutoka kwa wezi wanaoziuza kama vifaa kuu kuu ili kutokomesha uhalifu huo
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika la kuunganisha umeme mashinani amesema kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha wananchi wanaun ganishwa katika mfumo wa umeme na kuwataka wakaazi hao kuwatafuta mafundi waliohitimu kuwaunganishia umeme manyumbani mwao ili kupunguza visa vya hasara vinavyotokana na umeme
Imetayarishwa na Janice Marete