SERIKALI YATOA BILIONI 1.12 ZA UJENZI WA VITUO VYA KIBIASHARA

Serikali imetoa mgao wa shilingi bilioni 1.12 kufadhili mradi wa vituo vya biashara katika kaunti mbali mbali nchini.
Waziri wa biashara na viwanda Rebecca Miano amesema fedha hizo zinalenga kufadhili ujenzi wa vituo hivyo katika kaunti 17.
Miongoni mwa kauntu zitakazonufaika na fedha hizo ni Migori ,Mombasa,Busia ,Meru Bungoma Kirinyaga homabay Machakos siaya Kiambu muranga transnzoia embu uasiangishu nandi Nakuru na Garissa.
Kila kaunti itapata shilingi milioni 62.5.
Imetayarishwa na: Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































