WASHUKIWA WA KISUNZI CHA KOIMBURI WAPEWA DHAMANA
Mahakama ya Milimani imewaachia huru washukiwa wanne wanaohusishwa na madai ya utekaji nyara wa mbunge wa Juja George Koimburi kwa dhamana ya shilingi milioni 1 kila mmoja na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au bondi ya shilingi elfu 300 pesa taslimu.
Hakimu Carolyne Nyaguthii ametoa uamuzi huo amewazuia washtakiwa ambao ni mwakilishi wadi Grace Wairimu, Peter Gitau, David Macharia na Cyrus Muhia kuwasiliana na shahidi yeyote kwenye kesi hiyo.
Aidha, amewaagiza kumuona afisa wa uchunguzi Nicholas Njoroge kila wiki au kila watakapohitajika.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































