#Local News

EACC YAPONGEZA UAMUZI KUHUSU LENOLKULAL

Tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC imepongeza uamuzi wa mahakama inayosikiliza kesi ya ufisadi baada ya kumpata na hatia ya ufisadi aliyekuwa gavana wa Samburu Moses Lenolkulal na washtakiwa wenza 10.

Akizungumza nje ya mahakama ya Milimani baada ya uamuzi huo, msemaji wa EACC Eric Ngumbi amesema uamuzi huo una uzito mkubwa ikizingatiwa kwamba ni mara ya kwanza kwa kesi ya ufisadi inayomhusisha kiongozi wa haiba ya gavana kusikilizwa na uamuzi kutolewa.

Ngumbi amezungumza muda mfupi baada ya hakimu mkuu Thomas Nzioka kukubaliana na Ushahidi kwamba Lenolkulal alitoa tenda kwa kampuni yake kusambaza mafuta ya magari kwa serikali za kaunti hiyo alipokuwa madarakani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

EACC YAPONGEZA UAMUZI KUHUSU LENOLKULAL

MSIMAMIZI WA BAJETI APINGA OMBI LA SENETA

EACC YAPONGEZA UAMUZI KUHUSU LENOLKULAL

ISHARA YA DHAHABU YA ALAMISI KATIKA MBIO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *