OBURU ODINGA ; ‘RUTO MUST GO’ INAFUNGUA NJIA KWA GACHAGUA

Seneta wa Siaya Oburu Oginga alisema chama cha Orange Democratic Movement (ODM) kiko tayari kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na utawala wa Kenya Kwanza kwa ajili ya utulivu wa Kenya.
Akizungumza na wanahabari mjini Kisumu, Oburu alisema licha ya kuunga mkono msukumo wa vijana wa kizazi cha Gen-Z wanapaswa kufutilia mbali kauli mbiu yao “Ruto must go” kwa kuwa kulingana naye huenda zikasababisha taifa kwenye machafuko.
Oburu amedokeza kuwa hayuko radhi na uongozi wa Naibu Rais Rigathi Gachagua kutokana na mazungumzo yake ya ‘wanahisa’ hapo awali. Aliteta kuwa iwapo Rais William Ruto atatimuliwa, ni Gachagua ndiye atakayechukua nafasi hiyo.
Imetayarishwa na Janice Marete