ODM YAJITENGA NA MADAI YA UPINZANI

Chama cha ODM kimekana madai ya baadhi ya viongozi wanaoegemea mrengo wa Azimio kwamba kinahitilafiana na mchakato wa kubuniwa upya kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC, kikilaumu chama cha Wiper kutokana na kucheleweshwa kwa mchakato huo.
ODM kupitia kwa katibu wake mkuu Edwin Sifuna imejitenga na madai hayo kwenye kikao na wanahabari baada ya mkutano kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa chama hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa