MUDAVADI AISHUKURU UAE KWA KUTOA NAFASI ZA AJIRA KWA WAKENYA
Waziri mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi, ameshukuru Muungano wa Milki za Kiarabu UAE, kwa kutoa nafasi 30,000 za ajira kwa raia wa Kenya.
Mudavadi, ameelezea kujitolea kwa Kenya kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili pamoja na kupatikana kwa nafasi zaidi za ajira kwa wakenya walio na utaalam katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
Akizungumza wakati wa kikao cha nne cha tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Kenya na UAE, Mudavadi ametoa wito kwa nchi hizo mbili kuharakisha utekelezaji wa mkataba wa ushirikiano kuhusu leba wa mwaka 2018.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































