MSASA WA IEBC KUFANYIKA JUMAMOSI
Watu 7 walioteuliwa na Rais William Ruto kuhudumu kama mwenyekiti na makamishna wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC watapigwa msasa hapo kesho na kamati ya sheria na haki katika bunge la kitaifa JLAC, baada ya zoezi hilo awali kuzuiwa na mahakama.
Kupitia notisi ya umma iliyochapishwa kwenye magazeti ya humu nchini hii leo, karani wa bunge la kitaifa Samuel Njoroge amechapisha ratiba ya kikao hicho, mwenyekiti mteule wa IEBC Erastus Ethekon akiwa wa kwanza kufika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na George Muragara saa 3 asubuhi.
Zoezi hilo lilikuwa limeratibiwa kufanyika Jumatatu wiki hii ila mahakama ikazuia kwa muda, spika wa Bunge la kitaifa Moses Wetang’ula sasa akiitaka ikome kuingilia uhuru wa bunge.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































