GACHAGUA AELEKEA MAHAKAMANI KUPINGA KUBANDULIWA KWAKE MAMLAKANI
Katika juhudi za dakika za mwisho za kutaka kurejesha afisi yake, Rigathi Gachagua ameelekea mahakamani kumzuia Rais William Ruto kuteua naibu wake kujaza nafasi ya Naibu Rais.
Chini ya cheti cha dharura, Rigathi kupitia kwa Wakili Mkuu Paul Muite anashikilia kuwa mashtaka dhidi yake mbele ya bunge la kitaifa na baadaye Seneti hayana ushahidi.
Anasema Bunge la Seneti lilitakiwa kisheria kufanya kazi kama msuluhishi asiye na upendeleo katika kuzingatia iwapo mashtaka yaliyotangulia yamethibitishwa au la.
Anashikilia kuwa ushahidi uliotegemewa kuunda msingi wa kushtakiwa kwake haukutosha kufanya mchakato huo kuwa na dosari na kwamba yalikwenda kinyume na kiwango kilichowekwa na mahakama ya rufaa katika kesi ya Martin Wambora ambapo iliamuliwa kuwa katika masuala ya kumshtaki, madai lazima yawe mazito, makubwa na kwamba mashtaka kama yalivyopangwa lazima yafichue ukiukaji mkubwa wa sheria ambayo mawakili wa gachagua wanashikilia kuwa hakuna.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































