ADA YA MATIBABU YA KARIUKI YAZIDI KUONGEZEKA
Familia ya mchuuzi aliyepigwa risasi ya mpira na kuwaachwa na majeraha mabayaitahitajika kulipia ada ya matibabu inayozidi shilingi milioni 2.
Jamaa zake Bonface Kariuki wanasema mwanao ambaye angalia anatumia mitambo ya kumweka hai hawezi kuzungumza wala kuwaona na hali yake haijabadilika ada ya matibabu nayo ikifikia shilingi milioni 2.3.
Haya yanajiri huku mkuu wa polisi kupitia kamanda wa polisi eneo la kati Samuel Ndanyi aliyetembelea familia yake akitoa hakikisho kuwa lazima Bonface atapata haki,polisi 2 waliomkabili wakiendelea kuzuiliwa.
Imetayrishwa na Maureen Mukhobe
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































