GAVANA OTUOMA AWAONYA MAAFISA DHIDI YA SIASA
Visa vya maafisa wa umma kujihusisha na siasa wanapokuwa kwenye majukumu yao rasmi vimetajwa kuwa kizingiti kwa maendeleo katika kaunti ya Busia, gavana wa kaunti hiyo Paul Otuoma akiwaonya maafisa hao dhidi ya mienendo hiyo.
Akizungumza katika eneo la Budalang’i, Otuoma amelalamikia hatua ya maafisa hao kutumia raslimali za umma kuendesha siasa za mapema, na kuonya kuwa watakaopatikana watachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha, amewataka maafisa wanaojihusisha na siasa kujiuzulu.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































