SABABU YA NAIBU WANGU KUJIUZULU, GAVANA BII

Muda mfupi baada ya naibu gavana wa Uasin Gishu John Barorot kujiuzulu, gavana wa kaunti hiyo Jonathan Bii ameweka wazi sababu za naibu wake kuchukua uamuzi huo, akisema imetokana na Barorot kupata kazi katika shirika moja la kimataifa.
Katika kikao na wanahabari, Bii amesema kwamba naibu wake anafaa kuanza majukumu yake tarehe 1 mwezi ujao kama afisa mkuu mtendaji kwenye shirika hilo.
Aidha, amemtaja Barorot kuwa Rafiki yake, na kwamba wamefanya mazungumzo mara kadhaa kabla ya kujiuzulu kwake.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa