MASENGELI AAGIZWA KUJIWASILISHA MAHAKAMANI

Mahakama kuu ya Nairobi imemwagiza kaimu Inspekta Mkuu wa polisi Gilbert Masengeli kujiwasilisha mwenyewe mahakamani hii leo saa tisa kamili kujibu maswali kuhusu kupotea kwa watu 3 katika eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado yapata wiki 2 zilizopita.
Hii ni baada ya hakimu Lawrence Mugambi mnamo tarehe 28 mwezi jana kumwagiza Masengeli, mkurugenzi wa mashtaka ya umma, mwanasheria mkuu, mkurugenzi wa idara ya jinai DCI na idara ya ujasusi ya kitaifa kuweka wazi kwa chama cha wanasheria LSK kuhusu waliko watatu hao ambao ni Bob Michemi, Jamil Longton na Aslam Longton.
Hata hivyo, amri hiyo haikutekelezwa kwenye kesi iliyowasilishwa na LSK.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa