#uncategorized

BODI YA UTUMISHI WA UMMA BUSIA MOTONI

Mwenyekiti wa Bodi ya Utumishi wa Umma kaunti ya Busia Michael Onyura amekuwa na wakati mgumu kueleza madai ya kasoro na upendeleo katika uajiri wa hivi majuzi wa wakurugenzi na manaibu wakurugenzi wa idara mbali mbali.

Akiwa mbele ya Kamati ya Leba, Haki za Binadamu na Ustawi wa Jamii, ametakiwa madai kwamba kuna maafisa walioajiriwa bila kuteuliwa wala kuhojiwa kwa nafasi walizopewa, tuhuma ambazo amekanusha vikali.

Bodi hiyo aidha imetakiwa kueleza jinsi mtu asiye na uzoefu na ujuzi stahiki alivyopewa kuongoza idara moja muhimu.

Imetayarishwa na: Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *