HARAMBEE STARS KUPATA KOCHA HIVI KARIBUNI
Kocha mkuu mpya wa Harambee Stars huenda atateuliwa hivi karibuni kufuatia mkutano kati ya Rais wa FKF Hussein Mohammed na maafisa wakuu wa Wizara ya Michezo.
Waziri wa michezo Salim Mvurya na Katibu Mkuu katika wizara ya Michezo, Peter Tum wamesisitiza haja ya kuwa na kocha mwenye ujuzi wa kujenga timu ya ushindani kwa ajili ya michuano ijayo ya CHAN na AFCON 2027. Harambee Stars imekosa kocha wa kudumu tangu Engin Firat ajiuzulu Desemba mwaka jana, huku Francis Kimanzi akihudumu kwa muda.
Ratiba inayofuata ya timu ni ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026 mnamo Machi. Mjadala unaendelea kuhusu kubaki na Francis Kimanzi au kuteua kocha mpya kabla ya michuano ya CHAN mwezi Agosti.
Aliyekuwa kocha mkuu Jacob ‘Ghost’ Mulee hivi majuzi alishauri dhidi ya mabadiliko hayo, na kuitaka FKF kubaki na Kimanzi hadi baada ya CHAN. Majina kadhaa, akiwemo Benni McCarthy wa Afrika Kusini, yamehusishwa na jukumu hilo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































