WAZIRI KINDIKI AMEAGIZA WATU WANAOISHI KWA MISITU KUHAMA

Waziri wa usalama na maswala ya ndani prof Kithure Kindiki amewaagiza watu wanaoishi kwenye misitu kuondoka haraka.
Akizungumza mjini marsabit wakati alipoongoza shughuli ya upanzi wa miche , kindiki amesema ardhi kubwa ya misitu imenyakuliwa hali inayotishia usalama wa mazingira.
Kulingana na Waziri kindiki serikali itaendelea na mipango ya kuondoa watu wanaoishi karibu na mito akisema wamechangia pakubwa katika uharibivu wa mazingira