MAHAKAMA YASITISHA KAMATI YA UKAGUZI WA MADAI YA NHIF
Mahakama Kuu ya Eldoret imesitisha kwa muda shughuli za Kamati ya Ukaguzi wa Madai ya Matibabu ya NHIF hadi kesi ya kupinga uhalali wake itakaposikilizwa na kuamuliwa.
Jaji Nyakundi ametoa agizo la kuizuia kamati hiyo kuendelea na kazi yoyote, akisema waombaji wameonyesha hoja za msingi.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Dkt. Benjamin Magare na wengine, wakidai kuwa kamati hiyo ilibuniwa kinyume cha Katiba na kwamba kazi yake inakiuka mamlaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa tena Juni 2, 2025.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































