#Sports

KENYA KUANDAA FAINALI ZA CHAN

SHIRIKISHO la Soka barani Afrika (CAF) limetangaza nchi zitakazoandaa sherehe za ufunguzi na fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka huu.

Kenya imepewa haki ya kuandaa fainali, huku mechi ya ufunguzi ikifanyika nchini Tanzania.

Uganda itakuwa mwenyeji wa mechi ya mshindi wa tatu/nne kama ilivyotangazwa na CAF kupitia tovuti yao rasmi, baada ya mashauriano na nchi hizo tatu za Afrika Mashariki.

Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, Tanzania, utaanda mechi ya ufunguzi Jumamosi, Agosti 2, ambayo ina maana kwamba Tanzania itacheza mchezo wa kwanza wa michuano hiyo.

Uwanja wa Moi, Kasarani jijini Nairobi, utaandaa fainali na hafla ya kufunga mashindano Jumamosi, 30 Agosti.

Mchezo wa mshindi wa tatu/nne utafanyika kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole.

Kama sehemu ya dhamira ya CAF ya kupanua wigo na ushirikishwaji wa soka la Afrika, Zanzibar imeongezwa kuwa moja ya miji itakayoandaa CHAN inayofanyika kila baada ya miaka miwili

Imetayrishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *