#Athletics #Sports

HAKI YETU

Familia ya mwanariadha wa Uganda, Rebecca Cheptegei, ambaye alishiriki mbio za mita 10,000 kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka huu jijini Paris, Ufaransa imetaka hatua kali na za haraka zichukuliwe dhidi ya wahusika wa shambulio lililosababisha asilimia 75 ya majeraha ya moto mwilini mwake kufuatia madai ya mzozo kati yake na mpenzi wake Jumapili iliyopita.

Mwana olimpiki Cheptegei, ambaye anapigania uhai wake katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Moi Teaching and Referral jijini Eldoret, alishambuliwa katika makazi yake huko Kinyoro, eneo bunge la Endebess kaunti ya Trans-Nzoia mapema jumapili.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Bi Rose Chebet, mshukiwa, Dickson Ndiema Marangach, alimmwagia petroli kabla ya kumchoma moto punde tu alipowasili nyumbani kwake kutoka kanisani.

Wazazi wake, Agnes Cheptegei na Joseph Cheptegei wanasema hii si mara ya kwanza mshukiwa kumshambulia binti yao, huku makosa ya awali yakiripotiwa kwa mamlaka husika.

Katibu wa chama cha riadha nchini tawi la Trans-Nzoia Evans Rono alilaani kitendo hicho kiovu, akiwataka polisi kuharakisha uchunguzi.

Imetayarishwa na Nelson Andati

HAKI YETU

RAHEEM ASHABIKIA KUINGIA ARSENALI

HAKI YETU

KISIA AINGIA IMPALA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *