HATUJENGI TUKUPE, UTAPANGISHA- WAZIRI WAHOME
Ushuru unaotozwa kama mfanyakazi kugharamia mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu si wa kununua nyumba, bali ni wa kutumika kujenga nyumba hizo.
Ndiyo kauli ya waziri wa ardhi na nyumba Alice Wahome, akisema wakenya watahitajika kulipia kodi ya kila mwezi kuishi ndani ya nyumba hizo saw ana ilivyo kwa nyumba nyingine za kupanga.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha utangazaji, Wahome amesema wakenya watakaopata hizo nyumba watalipia kwa kipindi cha miaka 30.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































