RUTO AKUTANA NA VIONGOZI WA MAGHARIBI

Rais William Ruto amefanya kikao na viongozi wa eneo la Magharibi mwa nchi akiwemo spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, mawaziri Wycliffe Oparanya na Debora Mulongo, Pamoja na magavana wa eneo hilo isipokuwa Wilber Otichillo wa Vihiga, maseneta na wabunge.
Kulingana na taarifa kutoka Ikulu, mkutano huo umelenga kujadili masuala ya maendeleo hasa katika sekta za kilimo na usambazaji wa umeme.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa