#Football #Sports

CHELSEA YAKANYAGWA

Erling Haaland alifunga bao lake la 91 katika mechi yake ya 100 akiwa na Manchester City wakati mabingwa hao wakianza kutetea taji lao la Ligi ya Premia kwa ushindi mnono wa 2-0 ugenini dhidi ya Chelsea.

Nyota huyo mkubwa wa Norway, alimegewa pasi ya pesa na Bernardo Silva, na akalazimisha njia kati ya Marc Cucurella na Wesley Fofana na kumaliza kwa ustadi dhidi ya kipa Robert Sanchez dakika ya 18.

Kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Mateo Kovacic aliwahakikishia wageni ushindi dakika sita kabla ya mchezo kumalizika.

City, wakitafuta taji la tano mfululizo, walikuwa wametulia na mpira kuliko Chelsea na walionekana kutawala.

Lakini ilikuwa wazi kocha Maresca, ambaye alifanya kazi pamoja na Pep Guardiola katika klabu ya City kwa msimu mmoja kabla ya kuiongoza Leicester City kupanda Ligi Kuu mwezi Mei mwaka jana, ana kazi ya kufanya na kikosi chake kikubwa au kimrambe mapema.

Imetayarishwa na Nelson Andati

CHELSEA YAKANYAGWA

KABRAS RFC WABEBA KIKOMBE

CHELSEA YAKANYAGWA

NAIBU GAVANA WA KAUNTI YA UASIN GISHU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *