#uncategorized

SHERIA MPYA YA KUDHIBITI MUGUKA NA MIRAA MOMBASA

Serikali ya kaunti ya Mombasa imetoa notisi ya siku saba kwa wamiliki wa maduka ya reja reja jijini humo kuamua iwapo watafanya biashara ya kuuza miraa na muguka ama bidhaa nyingine.

Gavana wa kaunti hiyo Abdulswamad Shariff Nassir vile vile ametoa notisi hiyo kwa magari ya uchukuzi wa umma yanayosfirisha watu hadi momb asa kuamua iwapo wataendeleza biashara ya kuwasafirisha abiria, miraa ama muguka.

Amesema kuwa wafanyibiashara hao watapewa leseni maalum ya kuendesha biashara ya uuzaji wa bidhaa hiyo chini ya uangalizi wa kamati maalum itakayobuniwa na serikali ya kaunti ya kuhakikisha kwamba utafunaji wa miraa na muguka unadhibitiwa.

Hatua hiyo inalenga pia kudhibiti matumizi mabaya ya  bidhaa hiyo hasa miongoni mwa Watoto wenye umri mdogo ambao umekithiri katika kaunti ya Mombasa.

Haya yanajiri siku moja baada ya gavana wa Embu Cecily Mbarire kukutana na gavana wa mombasa Abdulswamad kujadili jinsi biashara hiyo itakavyoendelezwa jijini Mombasa bila Watoto kuadhiriwaKwa mujibu wa Mbarire serikali ya kaunti yake ipo tayari na maamuzi yatakayofanywa naserikali ya Mombasa ili kufanikisha hilo.

Imetayarishwa na: Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *