#Boxing #Sports

MACHARIA AINGIA KATIKA MABANO YA MEDALI

Bondia wa Kenya Clinton Macharia amefanikiwa kuingia kwenye mabano ya medali kwenye michuano ya masumbwi ya Afrika inayoendelea Kinshasa, DRC. Macharia, mchezaji mpya wa uzani wa super-heavy, alimtandika Luvo Jordilson wa Angola katika nusu-fainali kwa uamuzi wa pointi.

Hili linamhakikishia Macharia angalau medali ya fedha, huku macho yake yakiwa yameelekezwa kwenye dhahabu anapotinga fainali kumenyana na Younes Bouhdid wa Morocco.

Macharia, ambaye alianza safari yake ya ndondi mwaka wa 2019 katika Ukumbi wa Kijamii wa Kaloleni, hapa Nairobi alifurahishwa na wepesi wake na mchanganyiko wake ulioratibiwa vyema. Baada ya pambano hilo, Macharia alifichua kuwa Jordilson amekuwa akimtishia kwamba atamuangamiza ulingoni, lakini jana usiku alionyesha ari halisi ya kupigana ya Wakenya.

Kocha mkuu wa Kenya Musa Benjamin alionyesha furaha yake, akisema kwamba huo ni mwanzo tu wa mambo makubwa.

Wakati huo huo, macho yote yanaelekezwa kwa Abednego Kyalo, ambaye leo atamenyana na bingwa wa Mauritius, Fabrice Valerie katika nusu fainali ya uzani wa flyweight.

Imetayarishwa na Nelson Andati

MACHARIA AINGIA KATIKA MABANO YA MEDALI

KATIBU WA KNUT TAWI LA TRANSNZOIA GEORGE

MACHARIA AINGIA KATIKA MABANO YA MEDALI

GOR MAHIA WAKO TAYARI KWA MCHUANO WAO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *