POGBA ATANGAZA KUREJEA UWANJANI
Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa Paul Pogba ambaye amekuwa akitumikia marufuku kutokana na utumizi wa dawa za kusisimua misuli, amesema kwamba anafanya mazungumzo na klabu moja ili kuichezea.
Licha ya Pogba kukosa kuweka wazi klabu hiyo, walio karibu naye wanasema ni Monaco, na kurejea kwake kutakamilisha miaka 3 ya kukosa kusakata soka uwanjani.
Pogba aliyeichezea Manchester United ya Uingereza kabla ya kuondoka mwaka wa 2022, alirejea katika klabu ya Juventus nchini Italia ambako masaibu yake ya majeraha yalichukua mkondo tofauti na kuishia katika marufuku kutokana na utumizi wa dawa haramu.
Awali, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 alipigwa marufuku ya miaka 4 ila akakata rufaa na kupunguzwa hadi miezi 18, ambayo ilikamilika mwezi Machi mwaka huu.
Akizungumza na runinga moja nchini Ufaransa usiku wa kuamkia leo, Pogba ametaja kipindi hicho kuwa kigumu.
Imetayrishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































