CHIFU ATAKA KITUO CHA POLISI KUKABILI WIZI
Wakazi katika eneo la Ngweso kaunti ya Homa Bay wakiongozwa na chifu wa eneo hilo sasa wanaitaka serikali kujenga kituo cha polisi eneo hilo ili kukabili visa vya wizi hasa unaoelenga pikipiki kila siku ya soko.
Aidha, wamewataka polisi kuimarisha doria ili kukomesha visa hivyo ambavyo vimekithiri.
Wakazi hao wameyasema haya baada ya kumpiga hadi kufa mwanamme mmoja anayedaiwa kuwa mwizi sugu wa pikipiki baada ya kupatikana na pikipiki iliyopotea wiki moja iliyopita.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































