WANDAYI: TEKELEZA NADCO KABLA TUONGEE
Kiongozi wa walio wachache katika bunge la kiataifa Opiyo Wandayi amemtaka rais william Ruto kutekeleza ripoti ya kamati ya mazungumzo ya kitaifa NADCO kabla ya mazungumzo zaidi kufanyika.
Wandayi amesema kwamba muungano wa Azimio unaamini kwamba mazungumzo yanfaa kwa taifa ila utekelezaji wa ripoti hiyo utaashiria kujitolea kwa rais ruto kufanya mazungumzo kwa nia njema.
Aidha, Wandayi amesikitika kwamba ni iezi saba tangu kuwasilishwa kwa ripoti hiyo ila hadi sasa haijatekelezwa, akisema hilo linaashiria serikali haiku tayari kwa mazungumzo ya kitaifa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































