KENYA POLICE YASHINDA MARA SUGAR NA KUREJEA KILELENI MWA LIGI KUU YA FKF
Kenya Police waliwalaza Mara Sugar bao moja pekee na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Kenya (FKF) katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Awendo jana Jumapili.
Clinton Kinanga, ambaye yuko kwenye fomu bora, alifunga bao muhimu katika dakika ya 56 na kuwafanya maafisa wa polisi kurejea kileleni mwa ligi wakiwa na pointi 36, sawa na Tusker FC lakini wakiwa na tofauti nzuri ya mabao.
Hivi sasa, Police FC wako kwenye wimbi la ushindi baada ya ushindi wao wa ugenini Awendo kuwa wa tisa mfululizo chini ya kocha wa Kiburundi Etienne Ndayiragije, ambaye amesajili ushindi mara tisa na sare moja, akipoteza mara moja tu tangu kuchukua jukumu mwishoni mwa Novemba. Ushindi huo ulifuata baada ya mchezo mzuri wa 3-0 dhidi ya Bandari FC katika Uwanja wa Kenyatta Jumatano wiki iliyopita
Kwingineko, Gor Mahia walitoka sare ya bila kufungana dhidi ya Kakamega Homeboyz katika Uwanja wa Mumias.
Matokeo hayo yamepunguza matumaini ya Gor Mahia kutetea taji lao, huku Police FC wakifungua pengo la pointi nane dhidi ya Gor Mahia walio nafasi ya tatu, ambao wamecheza mechi moja pungufu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































