KENYA KUA WENYEJI KWA MASHINDANO YA DARTS

Kenya inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika ya Darts Continental Tour ambayo pia yatatumika kama Mashindano ya Kufuzu kwa michuano ya Dunia ya Vishale Afrika kuanzia Septemba 27 hadi 29 jijini Nairobi.
Mwenyekiti wa Kundi la Vishale la Buffalos Jeff Mureithi anasema michuano hiyo inaelekea kuvutia zaidi ya wachezaji 250 kote barani.
Mshindi atajinyakulia tiketi pekee iliyotengewa Afrika kwenye Mashindano ya Dunia ya Vishale ya PDC, sawa na Kombe la Dunia la mchezo wa vishale, yatakayofanyika nchini Uingereza Desemba mwaka huu.
Imetayarishwa na Nelson Andati