JUNET, ODHIAMBO WAIDHINISHWA.
Muungano wa Azimio la Umoja umeidhinisha uteuzi wa mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed kuchukua wadhifa wa kiongozi wa walio wachache katika bunge la kitaifa na kujaza pengo lilioachwa na Opiyo Wandayi.
Kupitia taarifa, chama cha ODM kimesema uamuzi huo umeafikiwa katikamkutano wa wajumbe wa Azimio.
Aidha, uteuzi wa mbunge wa Suba Kaskazini Millie Odhiambo kuchukua wadhifa wa kiranja wa walio wachacje bungeni umeidhinishwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































