KENYA, UHOLANZI ZASHIRIKIANA

Setkta ya kilimo nchini inatarajiwa kuimarika kufuatia udhabiti wa ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Uholanzi, mataifa hayo mawili yakitia Saini mikataba kadhaa ya ushirikiano ikiwemo kilimo.
Kutiwa Saini kwa mikataba hiyo kumewekwa wazi na Rais William Ruto katika Ikulu ya Nairobi ambako mfalme wa Uholanzi Willem Alexander na mkewe Malikia Maxima wamepokelewa.
Kwa upande wake, mfame huyo ambaye yuko ziarani nchini, amepongeza uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na taifa lake ambao umedumu kwa miaka Zaidi ya miongo 6.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa