APS BOMET YAPANDA HADI NAFASI YA PILI
APS Bomet imepanda hadi nafasi ya pili kwenye Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza baada ya kuichapa Vihiga United 2-0, mabao yakifungwa na Daniel Odhiambo na Lawrence Kibet.
Katika uwanja wa Serani, Mombasa United walirejea kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Luanda Villa kupitia mabao mawili ya Bakari Nyae na moja kutoka kwa Khamis Nyale huku Fidel Omondi akifunga bao la kufutia machozi kwa Villa.
Mechi hiyo ilisababisha mvutano dakika ya 83 baada ya bao la Villa kukataliwa, na mwamuzi kusitisha mchezo kabla ya dakika 90. Kocha wa Villa alilalamikia uamuzi huo huku Mombasa United wakisifu ushindi huo muhimu.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































