#Sports

ARTETA AFURAHISHWA KUIJIUNGA KWA NORGAARD KATIAKA KIKOSI CHAKE

Meneja wa Arsenal Mikel Arteta amefurahishwa na ujio wa Christian Norgaard, akisema kwamba analeta tajiriba ya uzoefu baada ya kusajiliwa na The Gunners kutoka Brentford leo.

Kiungo huyo wa kati wa Denmark mwenye umri wa miaka 31 amejiunga kwa ada ya awali ya Shilingi bilioni 1.9, kwa mujibu wa The Athletic.

Norgaard alifunga mara 13 katika mechi 196 akiwa Brentford na alikuwa mchezaji muhimu Brentford katika misimu minne iliyopita.

Anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Arsenal katika dirisha hili la uhamisho baada ya kiungo Mhispania Martin Zubimendi na kipa Kepa Arrizabalaga.

Arsenal pia wanaripotiwa kukaribia kumsajili mshambuliaji wa Sweden Viktor Gyokeres kutoka Sporting Lisbon.

Rais William Ruto leo amewakaribisha ikulu ya Nairobi timu ya Nairobi United, akiwapongeza kwa bidii yao na kuwataka kudumisha mwendo kasi wao kabla ya mechi yao ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya kushinda Kombe la FKF na taji la NSL.

Rais alibainisha kuwa ni onyesho la kipekee la timu hiyo, kushinda Ligi ya kiaifa ya daraja la pili na kuwashinda mabingwa wa msimu jana wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia katika fainali ya Kombe la FKF, na kujikatia tikiti ya kushiriki kombe la afrika.

Wakati huo huo wachezaji walieleza kuhusu kukumbatia utofauti na ushirikiano katika timu kwa matokeo yao bora msimu huu.

Imetayarishwa na Nelson Andati

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *