MMELEMAZA AFYA, AYACKO AISUTA HAZINA KUU
Gavana wa Migori Ochillo Ayacko ameikashifu hazina ya kitaifa kwa madai ya kuhujumu utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote kutokana na ukosefu wa fedha kwenye serikali za kaunti.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vituo vya afya kwenye kaunti hiyo, Ayacko amefadhaishwa na uchelewashaji wa mara kwa mara wa utoaji wa mgao wa kaunti na hivyo kulemaza huduma muhimu.
Aidha, amekariri kwamba kaunti zinakabiliwa na madeni na kufanya vigumu kutoa huduma kwa wagonjwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































