DCI HAIJIFAHAMU, WANDANI WA GACHAGUA

Wandani wa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua wamepuzilia mbali madai ya idara ya upelelezi DCI kwamba mbunge wa Juja George Koimburi alijiteka nyara, wakiwataja wanaoneza madai hayo kuwa wasiojifahamu.
Wakizungumza katika hospitali ya Karen ambako mbunge huyo anadaiwa kuendelea kupokea matibabu, viongozi hao wamemshutumu Inspekta mkuu wa polisi Dougalas Kanja kwa madai ya kuwahangaisha kutokana na uamuzi wao wa kumuunga mkono Gachagua.
Wakati uo huo, wabunge wameshinikiza Koimburi achukuliwe hatua za kisheria iwapo atapatikana na hatia ya kujiteka nyara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa