#Local News

EACC YAMKAMATA ALIYEKUWA DCIO WA LIKONI KWA TUHUMA ZA UFISADI

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa Wilaya ya Likoni (DCIO), Charles Onyango KA’galo.

Msemaji wa EACC, Eric Ngumbi, amesema kuwa KA’galo amekamatwa katika nyumba yake ya kijijini huko Oyugis. Na kwamba anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Port akisubiri kufikishwa mahakamani.

Ngumbi amesisitiza kuwa EACC imejizatiti kupambana na ufisadi katika ngazi zote za utumishi wa umma.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *