MOTO WATEKETEZA MALI YA THAMANI ISIYOJULIKANA EASTLEIGH

Mali yenye thamani isiyojulikana imeteketea baada ya moto unaokisiwa kutokana na kuvuja kwa mtungi wa gesi katika soko la Moonlight mtaani Eastleigh jijini Nairobi.
Wazima moto katika serikali ya kaunti ya Nairobi wamesaidia katika kuuzima moto huo.Akithibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Adamsom Bungei amesema kuwa hakuna majeruhi ambao wameripotiwa.
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































