SANDRO TONALI YUPO ANGEE

Newcastle United wamesema Sandro Tonali atapatikana tena kuanzia tarehe 28 Agosti kufuatia kupigwa marufuku kwa miezi 10 kwa kukiuka sheria za kamari.
Shirikisho la Soka la Italia (FIGC) lilimuadhibu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 mnamo Oktoba 2023 kwa kukiuka sheria inayokataza wachezaji kuweka dau kwenye ligi za shirikisho lao wenyewe, Uefa na Fifa wakati alipokuwa Italia.
Kiungo huyo wa kati wa Italia alijiunga na Newcastle kutoka AC Milan Julai 2023 na kufungiwa kwake kulikuja baada ya kucheza mechi 12 pekee na Magpies.
Imetayarishwa na Nelson Andati