BAENA AJIUNGA NA ATLETICO MADRID

Mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Alex Baena amesajiliwa na Atletico Madrid kwa mkataba wa miaka mitano, klabu hiyo ya La Liga ilitangaza Jumatano.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anawasili kutoka Villarreal kwa ada ambayo haijawekwa bayana, ingawa vyombo vya habari vya Uhispania vinaripoti kuwa dili hilo linaweza kufikia karibu euro milioni 50 ($58.8 milioni).
Alitumia msimu wa 2021/22 kwa mkopo Girona, kabla ya kurejea katika klabu yake kuu na kuimarisha nafasi yake kama sehemu muhimu ya ushambuliaji katika mabingwa wa Ligi ya Europa 2021. Baena amecheza mechi 10 za Uhispania na alikuwa sehemu ya kikosi cha La Roja kilichoshinda Ubingwa wa Ulaya msimu uliopita.
Imetayarishwa na Nelson Andati