#Local News

KAGWE AAHIDI KILIMO ‘SAFI’ KWA VIJANA

Wengi wa vijana nchini hawajihusishi na kilimo kutokana na mbinu zisizo na mvuto zinazotumika, nami nitahakikisha sekta hiyo inarekebishwa.

Ndiyo kauli ya waziri mteule wa kilimo Mutahi Kagwe, akizungumza alipofika mbele ya kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa kueleza ufaafu wake wa kuhudumu kwenye wadhifa huo.

Amesema kuwa iwapo ataidhinishwa, atashirikiana na wizara nyingine kuhakikisha wakulima wananufaika na kilimo.

Kuhusu suala lenye utata la chanjo ya mifugo, Kagwe ameahidi hamasisho kwa wafugaji kabla ya mpango huo kutekelezwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *