MHUDUMU WA BODA BODA, ABIRIA WAFARIKI BOMET

Mhudumu mmoja wa boda boda na abiria wake wamefariki dunia kufuatia ajali kaunti ya bomet.
Ajali hiyo imefanyika katika eneo la chebole barabara kuu ya Bomet-Kapulonga, wakati lori lililokuwa likitokea upande wa pili lilimgonga dereva wa pikipiki na abiria wake.
Akithibitisha kisa hicho kamanda wa polisi kaunti ndogo ya bomet ya kati Ali Bashir amesema wawili hao wamefariki dunia papo hapo.
Miili yao ilipelekwa katika hifadhi ya mahiti ya hosipitali ya rufaa ya Longisa.
Imetayarishwa na: Janice Marete