MAANDALIZI YA MASHINDANO YA KIP KEINO YATIA KASI
Huku saa zikiyoyoma kuelekea mashindano ya Kip Keino Classic ya Mei 31, maandalizi katika Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo yameshika kasi—na mkurugenzi Barnaba Korir anataka kasi hiyo iongezeke.
Korir, ambaye pia anahudumu kama mwenyekiti wa Maendeleo ya chipukizi wa shirikisho la riadha nchini (AK), amemtaka mwanakandarasi kuzingatia kuendesha kazi hiyo kwa saa 24 ili kuhakikisha kuwa zulia jipya liko tayari kwa mashindano hayo ya kifahari ya Continental Tour Gold.
Alitoa wito kwa Wizara ya Michezo kuingilia kati na kuharakisha mradi huo, akibainisha Kip Keino Classic imekuwa sehemu muhimu ya kalenda ya kimataifa ya riadha ya Kenya.
Rais wa AK Lt. Jenerali (Mst) Jackson Tuwei pia amekuwa akitetea azma ya Kenya kuandaa Mashindano ya Riadha ya Dunia siku za usoni, katika uwanja wa Nyayo au Kasarani. Kukamilika kwa uga wa nyayo kwa wakati kunaweza kuwa jambo kuu katika kuimarisha zabuni hiyo.
Imetayarishwa na Nelson Andati
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































