MAJAJI WADINDA KUJIONDOA KWENYE KESI YA GACHAGUA

Naibu rais aliyetuimuliwa kutoka mamlakani Rigathi Gachagua amepata pigo kwa mara nyingine mahakamani baada ya jopo la majaji 3 kudinda kujiondoa kwenye kesi yake jinsi alivyokuwa ameomba.
Katika uamuzi wao, majaji hao Anthony Mrima, Eric Ogola na Freda Mugambi wamesema gachagua ana haki ya kukata rufaa, na kuagiza kuwa kesi inayopinga kuingia afisini kwa naibu rais mteule Kithure Kindiki isikilizwe kuanzia tarehe 29 mwezi huu.
Hata hivyo, mawakili wa Gachagua akiwemo Danstan Omari wametofauatiana na uamuzi huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa