#Football #Sports

JUNIOR STARLETS WAIMARISHA MAZOEZI KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana Junior Starlets chini ya umri wa miaka 17 ,imeendeleza mazoezi yake  katika Jamhuri ya Dominica, kujiandaa kwa makala ya nane ya  fainali ya Kombe la Dunia .

Kenya maarufu kama Rising Starlets, watachezea mechi zao  mjini Santiago de los Caballeros ,wakifungua kampeini kundini C dhidi ya Uingereza Oktoba 17 ,kabla ya kuikabili Korea Kusini tarehe 20 mwezi huu, na kumaliza mechi za makundi dhidi ya  Mexico siku tatu baadaye.

Starlets waliwasili Dominican Jumatano lililopita baada ya kupiga kambi ya maozezi kwa wiki mbili nchini Uhispania.

Fainali za kombe la Dunia ambazo Kenya wanaofunzwa na Mildred Cheche wanashiriki kwa mara ya kwanza ,zitaandaliwa baina ya Oktoba 16 na Novemba 3 mwaka huu.

Imetayarishwa na Janice Marete

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *